Blog Details Home / Blog Details

Maafali ya Kidato cha Nne Shule ya Angelina Mabula 2025
Shule ya Angelina Mabula ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya maafali ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2025. Maafali haya yanatarajiwa kuwa ya kipekee, yakilenga kutambua juhudi na mafanikio ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari mwaka huu.
Mkuu wa shule, Mwalimu Joas Malima Maugo, ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na kamati mbalimbali zimeundwa kuhakikisha kila kitu kinakwenda kwa mpangilio mzuri. Alisisitiza pia kuwa maafali hayo yatakuwa nafasi nzuri ya kusherehekea mafanikio ya wanafunzi na kuhimiza bidii zaidi kuelekea mitihani ya taifa (NECTA).
Wanafunzi, walimu na wazazi wameonyesha hamasa kubwa katika maandalizi haya, huku mazingira ya shule yakipambwa kwa mandhari maridadi kuashiria tukio hilo muhimu linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Tunaendelea kuwakaribisha wazazi, walezi na wadau wote wa elimu kujiandaa kushiriki nasi katika sherehe ya maafali ya Kidato cha Nne 2025, tukio litakalobeba kumbukumbu ya kipekee katika historia ya Shule ya Angelina Mabula.
Leave A Comment
Sing in to post your comment or singup if you donβt have any account.
1 Comments
admin
1 month ago
Hongereni sana kwa maandalizi haya! π Tunatamani kuona siku ya maafali ikifika β bila shaka itakuwa siku ya furaha, fahari na mafanikio makubwa kwa wanafunzi wote wa Kidato cha Nne wa Angelina Mabula. Mungu aendelee kuwabariki walimu, wanafunzi na uongozi wa shule kwa kazi nzuri mnayoifanya. πβ¨