Blog Details Home / Blog Details

Walimu wa Angelina Mabula Wapokea Vyeti vya Pongezi kwa Mafanikio ya Kitaaluma
Walimu wa Angelina Mabula Wapokea Vyeti vya Pongezi
Uongozi wa Shule ya Sekondari Angelina Mabula unatoa pongezi kwa walimu wetu waliotambuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha ufaulu wa wanafunzi kwenye Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne (CSEE) mwaka 2024.
Kwa jitihada za pamoja, shule yetu imesaidia Halmashauri ya Ilemela kushika nafasi ya kwanza ya ufaulu katika Mkoa wa Mwanza. Walimu waliopokea vyeti vya pongezi ni:
- Mwl. Alberth Magere Munale – Somo la Physics
- Mwl. Julius Laurent Zacharia – Somo la Chemistry
- Mwl. Elliot Jacob Mayala – Somo la Biology
Vyeti hivi vimetolewa na Mhe. Hassan Masala, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, kwa niaba ya uongozi wa wilaya, kama ishara ya kuthamini mchango wa walimu wetu katika kuinua kiwango cha elimu.
“Niombe tuendelee kupambana ili vijana wetu wafanye vizuri zaidi mwaka huu. Ushirikiano wa walimu, wanafunzi, wazazi na jamii ndiyo nguzo kubwa ya mafanikio yetu.” – Kauli ya Mwalimu Mkuu.
Hongereni walimu wetu kwa heshima hii kubwa, na tunawatakia mafanikio makubwa zaidi siku zijazo.
Leave A Comment
Sing in to post your comment or singup if you don’t have any account.
0 Comments